Chama cha wafanyakazi madereva Tanzania-TADWU- kimetangaza
mgomo wa madereva nchi nzima kuanzia Agosti tisa mwaka huu baada ya wamiliki wa
mabasi, wakala wa usafiri wa nchi kavu na majini pamoja na wizara ya kazi
kushindwa kutekeleza makubaliano yalifikiwa na tume iliyoundwa na waziri mkuu
kutatua mgogoro wa madereva nchni.
Kauli hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wa TADWU, Bwana
Rashidi Salehe wakati akizungumza na Ripota wetu ambapo amesema mgomo huo
unarejea tena baada ya wamiliki wa mabasi kwa kushirikiana na wizara kazi
pamoja na Sumatra kuendelea kutumia mikataba ya zamani katika kutoa leseni
wakati makubaliano ya tume iliyoundwa na waziri mkuu yalitaka mikataba mipya
ianze kutumika kuanzia julai mosi mwaka huu.
Wakizungumza na Ripota wetu baadhi ya madereva wamelalamikia
wizara ya kazi na sumatra kwa kukaidi agizo la waziri mkuu na kuendelea kupokea
mikataba ya zamani toka kwa wamiliki wa mabasi na kutoa leseni wakati
makubaliano yalishafanyika na kusisitiza katika makubaliano hayo mishahara ya
madereva wa malori yanayotoka nje ya nchi walikuwa wanatakiwa kulipwa mishahara
ya shilingi milioni moja, huku madereva wa daladala shilingi laki tano pamoja
na posho nyingine.
Akizungumza kwa simu na mmoja wa viongozi wa chama cha
wamiliki wa mabasi nchni kwa masharti ya kutotajwa jina amewalalamikia madereva
hao kwa kupanga mgomo badala ya kupeleka madai yao kwa tume ya kudumu
iliyoundwa na waziri mkuu ili kupata ufumbuzi ambapo amesema kuna baadhi ya
madereva wanatengeneza migomo ili kuleta usumbufu kwa wananchi na serikali kwa
ujumla