F UFUGAJI WA NYUKI | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

UFUGAJI WA NYUKI

 Tanzania ina mazingira mazuri ya kuzalisha mazao ya nyuki kwa kuwa kuna mimea mingi ambayo inatoa maua yenye kutoa mbochi na chavua vitu ambavyo huwavutia nyuki na kutengeneza asali

Katika Tanzania mazao makuu yatokanayo na ufugaji wa nyuki ni asali na nta. Hata hivyo kuna mazao mengiambayo yanaweza kuzalishwa kutokana na asali na nta.

Tanzania tumejaliwa maeneo mengi sana na makubwa yenye misitu minene yenye chavua na nectar kwa wingi,maeneo hayo yapo karibu Tanzania nzima hayana matumizi yoyote yale ya ufugaji wa nyuki, kwa nchi nyingi Afrika kama vile Ethiopia na nchi nyinginezo ambazo zinasemekana kuongoza kwa ufugaji nyuki zinatamani sana maeneo mazuri tuliyonayo.

Maisha ya Nyuki

 Nyuki ni mdudu mwenye mabawa manne angavu na mwiba nyuma ya mwili wake anayekusanya mbewele ya maua kama chakula chake. Aina inayojulikana hasa ni nyuki wa asali wa familia apis. Kuna spishi zaidi ya 20,000 zinazojumlishwa na biolojia kati ya nyuki lakini wale wa jenasi apis wanaokusanya asali inayovunwa na wanadamu.

Nyuki za asali mara nyingi wanafugwa lakini wengine wanaishi porini na asali yaoinakusanywa kwa kuvunja mzinga wao. Katika Afrika kwa jumla sehemu ya asali bado inatokana na nyuki wa porini lakiniufugaji nyuki unapanuka

Hapo Mwanza wanajamii walikuwa wanafuga nyuki kwenye magome ya miti, vibuyu, vyungu, mapango, vichuguuna kwenye miamba. Baada ya muda ufugaji ulipiga hatua kidogo na watu wengi wakawa wanafuga kwa kutumia mizingailiyochongwa kutoka kwenye magogo ya miti. Ufugaji wa aina hii umedumu kwa karne nyingi kote nchini Tanzania


 Kutokana na uhitaji na ongezeko la matumizi ya bidhaa za nyuki, kulifanyika tafiti mbalimbali ambazo ziliweza kuboresha ufugajiwa nyuki kwa kuwa na mizinga ya kisasa ambayo imewezesha uzalishaji wa asali kuwa mkubwa na kuongeza pato la wafugaji tofautina ilivyokuwa hapo awali. Tafiti hazikuishia kwenye kuboresha mizinga tu, ila siku hadi siku kunavumbuliwanamna bora zaidi za kuimarisja uzalishaji wa nyuki

Hii ni aina mpya ya ufugaji wa nyuki ambao unaweza kujenga kibanda au nyumba kisha kuweka mizinga idadi unayohitaji.

Ni kwa nini kujenga nyumba au kibanda?

  • Ni muhimu kufuga nyuki kwenye kibanda au kwenye nyumba kwa sababu inasaidia kudhibiti wizi wa mizinga, pamoja na wanyamawanaokula asali na kudhuru nyuki
  • Inarahisisha utunzaji wa mizinga na kuwafanya nyuki wasihame kwenda sehemu nyingine
  • Inasaidia watu wengi kujifunza namna nzuri ya ufugaji wa nyuki, ikiwa ni pamoja na watoto, jambo ambalo linafanyashughuli hii kuwa endelevu
  • Ufugaji wa aina hii unasaidia kuwakinga nyuki dhidi ya majanga kama vile moto, na mafuriko.
  • Inawaepusha nyuki na usumbufu unaoweza kuwafanya wasizalishe kwa kiwango kinachotakiwa
  • Uzalishaji unaongezeka. Hii ni kwa sababu mizinga inayotumika ni ile ya kibiashara. Mzinga 1 unapata asali kilo 30 sawa na lita 20

AINA YA NYUMBA

Unaweza kujenga nyumba yenye upana wa futi 3 na urefu wa futi 9. Nyumba hii inaweza kuchukua mizinga hamsini. Halikadhalka, unaweza kujenga kibanda chenye ukubwa sawa na huo