Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za
uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha
jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu
yaani Bacteria.
Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris.Chunusi
ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano
nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni kumi na sa-ba..Chunusi
huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wa-kati wa balehe
(adolescents) .
Karibu asilimia 85 ya vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi
25 hupata chunusi na zaidi ya asilimia 20 ya wanawake wenye umri wa zaidi ya
miaka ishirini hupata chunusi wakati mwingine hata watoto wadogo pia huweza
kupata chunusi hii ni tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuwa chunusi ni
dalili ya balehe.
Chunusi ni ugonjwa unaoathiri vifuko au glandi za
ngozi.Katika ngozi ya binadamu kuna glandi ziitwazo Sebaceous ambazo zipo chini
ya ngozi na kazi yake kubwa ni kutoa mafutamafuta yaitwayo Sebum ambayo
hu-saidia kuiweka ngozi kuwa nyevu na yenye mvuto.
Wakati wa balehe mwili wa binadamu hutoa Sebum kwa wingi na
kwa sababu wakati huu vikemikali vya mwili yaani sex hormones hutolewa kwa
wingi hasa hormone ya kiume iitwayo androgen husababisha utoaji wa sebum kuwa
mwingi zaidi kuliko kawaida. Sebum inapotolewa kwa wingi huungana na seli za ngozi
zilizo-kufa na kutengeneza mchanganyiko mzito kama
nta uitwao comedo ambao huziba vishimo vya kutolea joto.
Maambukizi zaidi hutokea pale ambapo vijidudu yaani baktaria
vinaposhambulia vishimo vilivyoziba hapo kivimbe ambacho watu wengine huita Pimple
hujitokeza pale ambapo Sebum, bacteria, seli za ngozi na seli nyeupe za damu
zinapo-changanyika na kujikusanya katika vishimo vya jasho vilivyoziba na eneo
husika hupata vivimbe au vipele ambavyo tunaviita chunusi.
Ukubwa wa kipele hutegemea ngozi ya mtu au kiasi cha
mchanganyiko nilioeleza hapo juu katika eneo husika.Vipele vinaweza kuwa vidogo
au vikubwa. Chunusi wakati mwingine husababisha mabaka katika ngozi hali hii hutokea
pale ambapo seli za ngozi zilizoharibika huondolewa na seli mpya kutengenezwa.
Ngozi mpya
hutengenezwa kirahisi tu mahali palipokuwa na chunusi hali hii husababisha
mlingano usiosahihi wa ngozi na hutoa kidonda ambacho baadaye hubaki kama baka. Chunusi hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega
na mgongoni kwa sababu maeneo hayo yana vifuko au glandi za Sebaceous nyingi.
CHANZO CHA CHUNUSI
Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo baadhi ya
vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;
1. UMRI – Kama
nilivyosema hor-mone/vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa
kubale-he.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa nta (sebum) katika ngozi
ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
2. VIPODOZI –Baadhi
ya vipodozi kama Make-up za kina dada na
Sprays za ny-wele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi
zaidi.
3. CHAKULA- Chunusi
hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufan-ya chunusi kuwa nyingi
zaidi.
4. DAWA-Chunusi
zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile
antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,steroids na tranquilizers.Steroid ni
dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha
huzitumia tofauti na ma-kusudio ili kuongeza unene wa misuli yao.
5. MAGONJWA- Magonjwa
yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo
ya chunusi hasa kwa wasichana.
6. MAZINGIRA- Chunusi
huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye mafuta,grisi au hewa
chafu .Kutoa jasho sana
hasa katika mazingira ya joto huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.
7. JINSIA-Wavulana
hupata sana
chunusi kuliko wasichana.
8. FAMILIA- Wakati
mwingine chunusi hujitokeza sana
kwa wanafamilia wa familia kadhaa kuliko nyingine.
9. HOMONI- Mabadiliko
ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au
mwanamke anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata chunusi.
10. USAFI WA MWILI- Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa
chunusi au vipele hu-sababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na
jasho mwi-lini au kutooga huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi
11. MAWAZO AU STRESS-Mtu anapokuwa na mawazo mengi
vimkemikali kadha hutolewa mwilini ambavyo huwe-za kuchangia au kusababisha
chunusi
DALILI ZA CHUNUSI
Vipele au vivimbe vidogo vidogo ambavyo pengine husababisha
mwasho au vinavyouma ni dalili ya chunusi.Wakati mwingine huweza kujitokeza
kama baka dogo na wakati mwingine mtu anaweza utambuzi wa chunusi unaweza kuwa
mgumu kutokana na watu walivyomakini au wanavyojenga wasiwasi kubwa katika
mwonekano wao hasa usoni.Ikumbukwe kuwa kutokana mwonekano wa chunusi ni rahisi
sana
Daktari kuzigundua, japokuwa katika familia zetu ni mara
chache sana mtu
akaenda kumwona daktari au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa sababu ya
chunusi.Pale inavyotokea hivyo basi hali inakuwa ni mbaya zaidi.Hata hivyo si
vibaya kumwona daktari ambaye atakuuliza kuhusu chakula, ngozi, dawa unazotumia
na vitu vingine vinavyowe-za.kuchangia mtu kupata chunusi
MATIBABU
Matibabu ya chunusi yanajumuisha kupunguza utoaji wa anta
(sebamu ), kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani bacteria.
Matibabu huweza kutofautiana kutokana na wingia au ukubwa wa
tatizo. Suala la kuzingatia ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha chunusi kama nilivyoeleza hapo juu.
DAWA ZA KUPAKA
Kuna dawa za kupaka ambazo hupaka katika eneo la ngozi
lililoathirika kwa chunusi. Dawa hizi hupatikana kama
cream,lotion,gel au pad.
Dawa hizi hutumika kutibu chunusi ambazo haziko katika hali
mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo
tu. Mojawapo ya dawa hizi ni antibi-otic kama zenye mchanganyiko wa gentamyicin
na betamethasone au dexame-thasone kama vile Gentrisone au Gentriderm
cream,Erythromycin,B-Tex na kadhalika.Pia Persol forte Gel husaidia hasa
ukianza na asilimia ndogo (2.5%) na kuen-delea kadri ngozi yako inavyohimili
dawa. Gentamycin huua wadudu wanaosababisha chunusi wakati dawa nyingine
huondoa mwasho.
Dawa nyingine ni zile zinzolainisha nta au Comedolytics na
kufanya vishimo vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza kasi ya
utengenezwaji wa seli mpya za ngozi
Dawa hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara mbili au
tatu kila siku hasa baada ya kusafisha kwa maji safi na sabuni ya kawaida na kukausha kwa
taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua wiki kadhaa.
DAWAZA KUMEZA
Wakati mwingine daktari anaweza kumshauri mgonjwa kutumia
dawa za kumeza kulingana na wingi au ukubwa wa tatizo.
Dawa kama antibiotics huua wadudu na huzuia chunusi ,dawa
hizo ni kama vile Erythromycin topical,
Accutane (isotret-inoin), Benzamycin Cleocin T (clindamycin phosphate),
Desquam-E (benzoyl peroxide) Minocin (minocycline hydrochloride) na
”Si vema kujinunulia mwenyewe tu na kuanza kutumia bila
ushauri wa daktari au mtaal-amu wa magonjwa ya ngozi.”
Wanawake wenye chunusi zisizotibika wanaweza kupewa
Anti-androgens kama vile baadhi ya vidonge wa
uzazi wa mpango.Chunusi sugu hutibiwa kwa ciorticosteroids na anti-iflammatory
drugs ambazo hutibu chunusi sugu ambazo huitwa Acne fulminans na hupatikana zaidi
kwa vijana.
MATIBABU MENGINE
Kwa nchi zilizoendelea matibabu yanaweza kuwa hata upasuaji
mdogo (skin grafting) au plastic surgery kama chunusi imesaba-bisha baka kubwa
na kuna njia kama vile Chemical peel ambapo
kemikali hupakwa kwenye ngozi na inapokauka kipande au gamba la juu la ngozi
huondolewa na kuondoa baka.
MATIBABU MBADALA
Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga
mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya
ukavu nakuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.
Watu wenye chunusi wanashauriwa kulAa mlo kamili wenye
vyakula vyenye madini ya zinki,nyuzinyuzi, matunda, mboga za ma-jani,vitamin B
complex na Chromium. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya
maziwa, tumbaku, sukari, vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye
Iodine nyingi kama vile chumvi
MUHIMU
Chunusi haziwezi kutibika kabisa japokuwa iwapo matibabu
Yatakuwa sahihi watu 60 kati ya 100 hupona na unapokuwa unatumia dawa
usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi miwili kupata nafuu
na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia dawa.Chunusi pia huweza kupona kwa
kuacha mabaka ambayo kwa hapa nchini hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali
huweza kuondoka kadri muda unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa
na madhara katika ngozi.
MAMBO YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI
Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya
yafuatayo;
1. Osha taratibu
sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi
na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa
kucha au kitu choichote kigumu.
2. Tumia make-up au
vilainisha ngozi visivyo na mafuta mgando
3. Osha nywele zako
kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)
4. Kula mlo kamili na
epuka vyakula vyenye mafuta mengi.
5. Usibinye au kutoboa
vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.
6. Epuka kukaa sana juani,mwanga wa
asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D
7. Punguza mawazo