JESHI la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam limevunja kambi inayodaiwa kuendesha uhalifu wa kigaidi
wa kuvamia vituo vya polisi na kunyanganya silaha kwa ajili ya kuendeleza
uhalifu na kuweza kukamata watuhumiwa saba.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam,Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi
la Polisi (CP),Suleiman Kova amesema kundi limenaswa kutokana na taarifa
mbalimbali k mauaji ya kinyama na
uporaji silaha.
Amesema kundi hilo
linalodaiwa kuendeshwa na familia moja ya Ulatule limekuwa likiendesha matukio
mengi ya uhalifu ya kupora silaha katika vituo vya polisi.
Majambazi hao walikamatwa wakiwa na bunduki nne pamoja na risasi 18 aliwataja majina
watuhumiwa hao kuwa ni Saidi Mohamed Ulatule (67) ‘Uso a wa Simba’ , Mkazi wa
Mandimkongo, Mkuranga mkoa wa Pwani,Ramadhan Ngande (29)Miaka 29, Dereva wa
Bodaboda, Mkazi wa Kongowe,Hamis Ulatule (51),Mkulima, Mkazi wa Mamdimkongo,
Mkuranga, Pwani,Alli Ulatule(65), Mkazi wa Mamdimkongo, MKuranga, Pwani,Nassoro
Ulatule (40), Mkazi wa Mamdimkongo,
Mkuranga, Pwani,Seleman Ulatule (83),Mkazi wa Mamdimkongo, Said Chambeta (40)
‘Mzee wa Fasta’Mfanyabiashara wa Mitumba, Mkazi wa Yombo Makangarawe kati yao
Mtuhumiwa wanne ni wa familia moja inayojihusisha na vitendo vya ujambazi
pamoja na vya kigaidi.
Wakati huo Jeshi la Kanda Maalum ya Dar es
Salaam,limewakamata watuhumiwa sita wa mauaji wa Askari wa kikosi cha kupambana
na uhalifu Morogoro,Elibariki Pallangyo lilolofanyika nyumbani kwa marehemu
Mbagala jijini Dar es Salaam.
Kova amesema katika tukio la kukamata watu hao kiongozi wao,
Omary Salehe (Bonge Mzito) alisema kuna silaha ikiwa ni njia ya kutaka kutoroka
katika mikono ya polisi ambapo polisi walitumia mafunzo yao vizuri na kufanikisha kumjeruhi na
alifariki wakati akipelekwa Hospitali.
Wengine ni Said Mazinge (37) Mkazi wa Tegeta Kibaoni
Rashid Watson (21)‘Dodo’Mkazi wa Vingunguti, Ramadhan Salum (38)’Nguzo Mkazi
wa Mbagala Kiburugwa Bakari Rashidi (38) ‘Malenda’ Mkazi wa Mbagala kizuiani Hamis Hamis (24)
‘Freemason Mkazi wa Mbezi .