F Mtoto aliwa na Mamba Geita Alikuwa akiosha vyombo na wenzake ziwani | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mtoto aliwa na Mamba Geita Alikuwa akiosha vyombo na wenzake ziwani

Mtoto Avelina Vitus (8) mkazi wa kijiji cha Chelameno kata Nyamboge  wilaya na Mkoa wa Geita amefariki dunia baada ya kukamatwa na mamba pembezoni mwa ziwa Victoria juzi.

Wakizungumza na Channel Ten iliofika kijijini hapo na kukuta wananchi wakiwa kwenye mitumbwi wakimsaka mamba huyo wamesema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 10:30 jioni  katika kijiji hicho.

Wamesema mtoto huyo akiwa na wenzake katika mwalo wa Mchungwani mwambao wa ziwa hilo wakiosha vyombo mamba alimdaka msichana huyo na kutoweka naye na hapa wanaeleza
Baadhi ya wananchi akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mazura Luhibachi, walijitokeza kumtafuta kwa muda wa siku tatu bila mafanikio, huku wakiitupia lawama Idara ya Maliasili na Mazingira kwa kushindwa kumuua myama huyo ambaye amekuwa ni kero kwao.