F Kifua Kikuu kinauwa Watanzania 12,000 kila mwaka | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kifua Kikuu kinauwa Watanzania 12,000 kila mwaka

Waziri mwalimu amesema Takwimu za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa mikoa 12 nchini ikiongozwa na mkoa wa Arusha inachangia zaidi ya Asilimia 70 ya wagonjwa wote wa kifua kikuu Tanzania Bara na Visiwani.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na asasi ya kimataifa ya wadau walio katika mapambano dhidi ya ya kifua kikuu duniani(IUATLD)Takwimu zinaonyesha kuwa kwa Tanzania takribani watu 12000 hufariki kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu kila mwaka.

Hayo yamesemwa na waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akitoa tamko la serikali kwenye maadhimisho ya siku ya kifua kikuu Duniani ambayo hufanyika Trh 24.03 kila mwaka.

Waziri mwalimu amesema Takwimu za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa mikoa 12 nchini ikiongozwa na mkoa wa Arusha inachangia zaidi ya Asilimia 70 ya wagonjwa wote wa kifua kikuu Tanzania Bara na Visiwani na kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita wastani wa wagonjwa wapya 63000 wamekua wakigundulika na kuanzishiwa matibabu.

Amesema ili kuhakikisha ugonjwa huu unatokomea serikali imeanza kupeleka matibabu ya kifua kikuu hadi ngazi ya Kaya na kwakuwafikishia wagonjwa dawa majumbani kwao na kuwahamasisha wamiliki wa shule kuwafanyia vipimo wnafunzi mara kwa mara.

Kwa Upande wake Meneja wa mpango wa Taifa wakudhibiti Kifua kikuu na Ukoma Dr.Beatrice Mutayoba amesema kuwa Tafiti zinaonyesha kuna uwezekano mkubwa wa wazee na watu wanaoishi vijijini wanaonyesha wanauwezekano mkubwa wakuugua Kigua kikuu.