Mbeya. Diwani wa Kata ya Isyesye, Ibrahimu Mwampwani (Chadema) na Mwenyekiti wa Mtaa wa Manga Veta, Godlove Haule (Chadema) nusura watwangane makonde mbele ya wananchi baada ya kutuhumiana kula rushwa kutoka kwa mwenye jengo la ghorofa linalodaiwa kujengwa juu ya mkondo wa maji na kusababisha mafuriko jijini Mbeya.
Sakata hilo lilitokea baada ya viongozi hao kukutana mbele ya jengo hilo wa kiwa na baadhi ya watendaji wa halmashauri na wananchi wakijadiliana jinsi yakukabiliana natatizo la mafuriko yanayotokea mara kwa mara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha .
Akizungumziatukiohilo, John Steven mkazi wa Isyesye alisema kuwa walifika katika eneo hilo kwalengo la kupata suluhisho la mafuriko na ubovu wa miundombinu ya barabara kwani limekuwa nitatizo kubwa katika eneo hilo ambapo asilimia kubwa ya wananchi wanaokaa eneo hilo wameyafungia ndani magari yao kutokana na kushindwa kupita.
“Hawa ni viongozi wetu na ndiyo wanashughulikia suala hili lakini cha kushangaza inaonyesha baadhi yao wanamaslahi binafsi hadi wanafikia hatua kama hii yakurushiana maneno na kutaka kupigana wakati tunaoumia ni sisi wananchi wa kawaida kutokana na mafuriko,” alisema
Haule alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema kuwa ni kweli walitaka kurushiana makonde kutoka na na baadhi ya viongozi wa kisiasa wamekuwa wakifanya kazi kwa maslahi yao kwani tatizo la jengo hilo la ghorofani la muda mrefu lakini hakuna hatua inayochukuliwa.
Kwa upande wake Mwampwani alipoulizwa kuhusiana natukio hilo alisema kuwa ni kweli hali hiyo ilikuwepo ni baada ya kuambiwa na mwenyekiti huyo kuwa inawezekana atakuwa amechukua rushwa kwa mmilikiwa jengo hilo.