F HISTORIA YA PESA ZA NOTI ZA TANZANIA ..PART 2 | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

HISTORIA YA PESA ZA NOTI ZA TANZANIA ..PART 2

1 Zanzibari Rupee

Baada ya utawala wa kijerumani kuanguka na nchi kuchukuliwa na waingereza, kwanza nchi ilitumia noti za Rupee za Afrika ya Mashariki na Rupee za Zanzibar ingawa Rupie za kijerumani pia ziliendelea kutumika. Kwa upande wa Zanzibar noti ya rupee 1 ilianzishwa mwaka 1920. baadhi ya noti hizo ni hizi hapa

1 EA Rupee

5 EA Rupee

10 EA Rupee

Katikati ya mwaka 1920, serikali ya uingereza ilianzishwa sarafu ya pamoja kwa nchi zote za Afrika ya Mashariki iliyojuliakana kama Florin ya Afrika ya Mashariki. Noti za Florini zilikuwa katika thamani za Florin 1, 5, 10, 20, 50, 100 na Florin 500, ambapo noti za kuanzia Florin 10 na kuendelea juu zilikuwa pia na thamani ya Pound (1, 2, 5, 10 na 50). Kwa vile sarafu hii haikudumu zaidi ya miezi sita, ni noti chache sana zilizotolewa, mifano ya noti hizo ni kama ifuatavyo

1 EA Florin

5 EA Florin

Mwanzoni mwa mwak 1921, serikali ya kiingereza ilianzisha sarafu ya pamoja afrika mashariki iliyojulikana kama Shillingi ya Afrika ya Mashariki na hivyo kuondokana na Florin ya Afrika Mashariki. Shilingi ya Afrika Mashariki (baadaye nitakuwa naandika kwa kifupi tu kama Shilling) ilikuwa na thamani ya Shillingi 20 kwa pound moja na ilikuwa imeegeshwa kwenye pound kiasi kuwa thamani ya Shilling 20 kwa pound haikubadilika. Noti za Shillingi zilizotolewa wakati huo zilikuwa za thamani za Shillingi 5, 10, 20, 100, 1000, na Shillingi 10,000. Noti za Shillingi ishirini na kuendelea juu zilikuwa pia na thamani ya pound (1, 5, 50). Noti hizi zilikuwa zimeandikwa kwa kiingereza, kiarabu na kiamhara kinachotumika Ethiopia. Katika utawala wote wa kiingereza, kulitolewa mitindo miwili tu ya noti hizo. Mtindo wa kwanza ulidumu kuanzia mwaka 1921 hadi mwaka 1958, ma mtindo wa pili ulidumu kuanzia mwaka 1958 hadi baada ya uhuru mwaka 1964. Sura ya mbele ya noti zote ilikuwa ikionyesha mtawala wa himaya ya uingereza. Sura ya nyuma kwa upande wa noti za mtindo wa kwanza ilikuwa na simba mmoja wa kiume katika eneo la mlima Kenya. Noti zilizotolewa mara ya kwanza wakati wa utawala wa Mfalme George wa tano (1910-1936) ni kama ifuatavyo:


5 EA Shilling

10 EA Shilling


20 EA Shilling

100 EA Shilling


1000 EA Shilling

(Picha hii ilipingwa wakati pesa imeshafutwa rasmi kwa kutobolewa matundu; noti halisi haikuwa na matundu hayo)

Kwa thamani ya shillingi na uchumi wa watu wakati huo, ni noti chache sana zenye thamani ya Shilling 1000 na Shillingi 10,000 ziliingia kwenye mzunguko, na sikufanikiwa kupata noti ya Shilingi 10,000. Kwa hiyo ilipofika mwaka 1933, serikali ikaamua kusimaisha matumiz ya noti za shillingi 1000 ingawa zile za shillingi 10,00 ziliendelea. Wakati wa utawala mfupi wa Mfalme Edward wa nane mwaka 1936, hazikutolewa noti zozote. Noti nyingine zilitolewa wakati wa utawala wa mfame George wa sita (1936-1952), ambapo noti ya Shillingi 1 ilianzishwa. Noti hizo zilikuwa kama ifuatavyo.

1 EA Shilling

5 EA Shilling

10 EA Shilling

20 EA Shilling

100 EA Shilling

Kutokana na uhadimu wake, sikuweza kupata noti za Shillingi 10,000. Hata hivyo miaka 11 ndani ya utawala wa mfalme George wa sita, iliamuliwa kufuta noti hizi za Shillingi 10,000 ambazo zilikuwa hazitumiki sana. 

Baada ya kifo cha Mfalme George wa sita mwaka 1952 na binti yake Malkia Elizabeth wa pili kuchukua usukani noti zilizotolewa zilikuwa zinafanana na zile zilizokuwapo mwazoni isipokuwa aliondoa noti ya Shillingi 1 kwenye mzunguko.

5 EA Shilling



10 EA Shilling

20 EA Shilling

100 EA Shilling


.... INAENDELEA​