F JINSI YA KUPIKA PIZZA JIFUNZE HAPA | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

JINSI YA KUPIKA PIZZA JIFUNZE HAPA


  1. Unga 4 Vikombe

  2. Maziwa ya unga 2 vijiko vya supu

  3. Mafuta ya zaituni ½ kikombe

  4. Hamira 1 kijiko cha supu

  5. Chumvi kiasi

  6. Sukari 1 kijiko cha chai

  7. Maji dafu dafu 2 kikombe

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA UNGA
1. Changanya vitu vyote katika bakuli na ukande unga.
2. Ufunike na uache uumuke.


SOSI YA PIZZA

  • Kitunguu kilichokatwa kidogo kidogo 1
  • Thomu iliyokatwa ndogo ndogo 3 chembe 
  • Sosi ya HP 3 vijiko vya supu
  • Sosi ya tomato 3 vijiko vya supu
  • Pilipili manga 1 kijiko cha chai
  • Oregano ½ kijiko cha chai
  • Parsley (ukipenda) ½ ukipenda



1. Kaanga vitunguu kisha tia thomu, na vitu vyote iwe sosi.

2. Epua kwenye moto.


UPENDAVYO KATIKA HIVI AU VYOVYOTE VINGINEVYO


  • Tuna 
  • Nyama ya kusaga iliyopikwa 
  • Kuku aliyekaushwa na kukatwa vipande vipande 
  • Sauage zilizokatwa 
  • Salami 
  • Vipande vya nanasi 

VITU VYA KUJAZA JUU YA PIZZA

  • Nyanya zilizokatwa vipande vipande
  • Pilipili mboga iliyokatwa ndogo ndogo
  • Zaituni ikiwa za kijani au nyeusi


Cheese ya Mazorella
1. Fanya madonge madogo madogo kisha usukume kidogo tu size kama kwenye picha.
2. Paka sosi juu ya unga
3. Tia kiteo upendacho
4. Mwagia vitu vya kujaza juu ya pizza
5. Mwagia cheese
6. Pika katika oveni kwa muda dakika 20 au zaidi hadi ziwive pizza.