F Halmashauri ya wilaya ya Tarime yakataa kupokea Madawati yaliyotengezwa chini ya kiwango. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Halmashauri ya wilaya ya Tarime yakataa kupokea Madawati yaliyotengezwa chini ya kiwango.

Halmashauri ya mji wa Tarime mkoani Mara, imekataa kupokea idadi kubwa ya madawati baada ya kubaini kuwa madawati hayo yametengenezwa chini ya kiwango huku halmashauri hiyo ikiwa tayari imetumia mamilioni ya fedha za kodi za wananchi kumlipa mkandarasi aliyeteuliwa kufanya kazi hiyo.

Akizungumza baada ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inatekelezwa katika mitaa ya mji huo, baada ya halmashauri hiyo kugawanywa kutoka kwa iliyokuwa halmashauri ya Tarime, mwenyekiti wa halmashauri ya mji Tarime Bw Khamis Nyanswi, amesema katika ukaguzi huo wamebaini madawati hayo ambayo mengi yamesambazwa katika shule za msingi na sekondari, yametengenezwa chini ya kiwango.

Naye mbunge wa jimbo la Tarime mjini Mh Esther Matiko, akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo, amepongeza usimamizi mzuri wa fedha zinazotolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri ya mji wa Tarime, ambayo inaongozwa na chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema.