Diwani wa kata ya Chifunfu Robert Madaha amesema wataendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria,wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kuvua samaki kwa kutumia zana haramu,yakiwemo makokoro na nyavu za timba zilizopigwa marufuku na serikali.
Baadhi ya wakazi wa kisiwa hicho wameiomba serikali kuliangalia upya suala la uvuvi haramu kwani umekuwa ni tishio kwa raslimali za uvuvi endelevu na hata kusababisha kupungua kwa pato la wavuvi kutokana na kupungua kwa samaki.
Kitongoji cha Lyakanyasi ni muungano wa visiwa vitatu vya Biswa, Nyanzune na kisiwa cha Lyakanysi vyenye jumla ya wakazi 3000 ambao shughuli zao za kila siku ni uvuvi.