F TANGAZO: Shule ya Sekondari Realhope iliyopo Mafinga Iringa inawatangazia Nafasi za masomo kwa Bweni na Mchanganyiko | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

TANGAZO: Shule ya Sekondari Realhope iliyopo Mafinga Iringa inawatangazia Nafasi za masomo kwa Bweni na Mchanganyiko

Shule ya sekondari Realhope Mafinga yenye usajili namba s. 4885. Shule inapatikana Kinyanambo “C” eneo la makwawa. Shule inatangaza nafasi za kujiunga na elimu ya sekondari kwa mwaka wa masomo, january 2017 kwa kidato cha kwanza na nafasi chache za kidato cha pili.

Ni shule ya bweni na ya mchanganyiko (wasichana na wavulana) shule inapokea wanafunzi toka dini na madhehebu yote , walio tayari kulelewa na kukuzwa kwa maadili ya kanisa takatifu katoliki, na ni ya mchepuo wa sayansi na sanaa.

Fomu za maombi zinapatikana maeneo yafuatayo : Ofisi za parokia Mafinga ,Dick hardware Kinyanambo “B” ,Chuma stationery Kinyanambo “B” ,Mwipopo hardware karibu na Mapanda hotel ,Mr bookshop Mafinga na Sub stationery Mafinga sokoni,kwa gharama ya Tsh 15,000/=
Pia unaweza kupata form kupitia website ya shule: realhopesecondaryschool.blogspot.com

Mtihani wa usahili utafanyika tarehe 17/09/2016  na Tarehe 24/09/2016 Jumamosi saa tatu asubuhi shuleni realhope.

Malipo ya fomu  yalipwe kwa M-pesa 0764-037385 na ujumbe utumwe kwenye namba hii pamoja na jina la mwanafunzi.

Masomo ya awali (pre-form one) yataanza tarehe 3/10/2016 hadi tarehe 10/12/2016 (wiki kumi)
Kauli mbiu yetu ni sala, nidhamu na kazi        
      

CONTACT US   0767147677 - 0767601318 - 0755214887 Huduma zetu ni zauhakika  Nyote mnakaribishwa.