F Paul Makonda amfungukia Mke wake Instagram | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Paul Makonda amfungukia Mke wake Instagram


Wakati mwingine sio vibaya kumuonesha mwenza wako namna gani unafurahia uwepo wake na thamani yake katika maisha yenu ya kila siku, inawezekana kufanya hivyo kunaweza kuongeza upendo kama alivyo fanya Mkuu wa mkoa wa Jiji la Dar es salaam Paul Makonda kwa mkewe Maria kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika hivi

"Najua nina WEWE na hiyo INATOSHA!

Wewe ndio siri ya NGUVU YANGU, wewe ndio kila kitu kwenye maisha yangu.. najua nimewahi kukukosea lakini ninachofahamu hata wakati nakukosea bado ulikuwa mwanamke pekee ninaekupenda, hakuna aliewahi kuzidi thamani yako, na nakuaminisha leo HATATOKEA!! Vingine ni ubinaadamu tu lakini haina maana kuna mbora zaidi yako, Huenda ubinaadamu huohuo kwa mwingine angeshindwa na kunikatia tamaa, lakini HUKUNIACHA, ulikuwa upande wangu, hata pale nilipokupa huzuni bado FURAHA YANGU ndio kitu cha kwanza ulichokiangalia, kama MAMA anavyomtizama mtoto ndivyo ulivyokuwa ukinitazama, na bado hukuacha kuniombea kwenye kila ninalolifanya, wewe ni wa thamani kubwa sana kwangu, nashindwa jinsi ya kumshukuru MUNGU kwa uwepo wako ndani ya maisha yangu, nilipofeli ulikuwepo, ninapofaulu upo na hata Dunia yote inizomee najua nina mtu ambae thamani yangu bado ni KUBWA mbele ya macho yake ambayo haitaka ishuke hata mbingu na ardhi vigeuke, 

Katika anniversary yetu hii leo tukiwa tunatimiza miaka MITANO ya ndoa yetu, bado sura ya kwanza inayonijia machoni kila ninapoamka ni YAKO!! Mapenzi yangu kwako ni ya pekee kiasi hata nakosa cha kufananisha nayo' na yanazidi kuongezeka kila iitwayo siku.

Huenda kuna muda nakukera, I am not perfect mimi ni binaadamu tu, na labda sina kila unachokihitaji, lakini unachotakiwa kujua ni kwamba NINA MAPENZI YA KWELI KWAKO, na niko tayari nipoteze kilakitu lakini SIO WEWE.

Naomba MUNGU akulinde na kukupa uhai mrefu ili niendelee kukuona kila siku za maisha yangu, na zaidi naomba MUNGU atulindie ndoa yetu na kutuepusha na kila linaloweza kuweka Doa, natamani niendelee kuelezea Dunia wewe ni wa thamani kiasi gani kwangu, lakini sidhani kama MANENO YANGU yataweza kufika hata robo ya ninachotaka kumaanisha, kuna mengi nayaona ndani yako, lakini kwa kifupi tu nataka nikwambie kuwa 
NAKUPENDA SANA MKE WANGU MARIA"