Pembe za ndovu
Maafisa wa forodha wa Vitenam wamenasa karibu tani moja ya pembe za ndovu zilizokuwa zimefichwa katika shehena ya mbao kutoka Kenya.
Taifa hilo la kikomunisti ni kituo maarufu kinachotumiwa katika usafirishaji wa pembe za tembo kutoka Afrika kuelekea maeneo mengine ya Asia, hasa China, ambako zinatumika kwa urembeshaji na kwa ajili ya kutengeneza dawa.
Bidhaa zinazotengenezwa na pembe za ndovu pia ni maarufu Vietnam ingawa biashara hiyo kisheria imepigwa marufuku.
Source: Eatv