F Chelsea yapeta bila Diego Costa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Chelsea yapeta bila Diego Costa

Vinara wa ligi kuu ya England, Chelsea waliendelea kujikita kileleni kwa kuwachakaza mabingwa watetezi Leicester City kwa mabao 3-0 bila ya mshambuliaji wake tegemezi ambaye inasemekana ana matatizo Na benchi la ufundi, Diego Costa.
Tokeo la picha la diego costa
Chelsea walipata mabao yao kupitia Marco Alonso aliyeingia kambani mara mbili, huku mshambuliaji wa kihispania Pedro akimalizia msumari wa mwisho kwa kupachika bao la tatu.

Matokeo ya mechi za awali Spurs na Arsenal walipaata ushindi wa goli 4 kila mmoja. Spurs walichakaza Westbromwich kwa mabao ya Harry Kane aliyefunga mara tatu ‘hat-trick’ na goli la kujifunga la G McCauley. Magoli ya Arsenal yalifungwa na Olivier Giroud, Alexis Sanchez na magoli mengine ya kujifunga ya J. Cork na K Naughton.

Kwingineko nchini Hispania Lionel Messi Na Suarez waliongoza mauaji dhidi ya Las Palmas kwa ushindi wa mabao 5-0, Suarez – 2, Messi – 1, A.Turan – 1 na A.Vidal – 1.

Matokeo mengine: Burnley 1-Soton 0 , Hull City 3-B’mouth 1, Westham 3-C.Palace 0, Watford 0- M’boro 0,Sunderland 1- Stoke 3.