F Kocha Wa Zamani Wa Boban Ana Nafasi Kubwa Yakumsaidia Ulimengu Sweden | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kocha Wa Zamani Wa Boban Ana Nafasi Kubwa Yakumsaidia Ulimengu Sweden

 Mshambuliaji Mtanzania, Thomas Ulimwengu ana nafasi kubwa ya kufanya vema katika Ligi Kuu ya Sweden kwa kuwa anakutana na mmoja wa makocha bora nchini humo.

Perre Ollson ndiye Kocha Mkuu wa AFC, kocha huyo aliwahi kumfundisha Haruna Moshi ‘Boban’ katika kikosi cha Gefle IF cha Sweden.

Ollson kwa sasa ndiye kocha wa AFC na inaelezwa ni mmoja wa makocha wanaokuza na kuendeleza wachezaji chipukizi kwa wingi, ingawa alichemsha kwa Boban.

Mfumo wa Ollson ni kutoa nafasi zaidi kwa vijana wenye vipaji kukuza na kuviendeleza vipaji vyao.

Tayari Ulimwengu ameanza mazoezi chini ya kocha huyo huku Mtanzania huyo ikiwa amerejea Sweden katika timu hiyohiyo ya AFC ambayo kwa mara ya kwanza alipelekwa na wakala Mtanzania wakati huo, Dkt Damas Ndumbaro.