F Mkurugenzi Mtendaji metoa siku 14 kwa Kampuni ya Nella Construction CO. Ltd kumalizia ujenzi wa Daraja | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mkurugenzi Mtendaji metoa siku 14 kwa Kampuni ya Nella Construction CO. Ltd kumalizia ujenzi wa Daraja

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Misungwi ,ametoa siku 14 kwa Kampuni ya Nella Construction CO. Ltd kuhakikisha wanakamilisha Ujenzi wa Daraja katika barabara ya Mbarika -Ilujamate -Mwawile yenye urefu wa kilomita 46.5 inayohudumia wakazi wa Kata ya Mbarika, Lubili, Isenengeja na Nhundulu.

Mkurugenzi Mtendaji huyo, Ndg, Eliurd Mwaiteleke aliagiza Idara ya Ujenzi kufuatilia kwa karibu mradi huo ambao umechukua muda mrefu bila kukamilika pamoja na Halmashauri kuongeza muda wa kazi kwa Mkandarasi huyo toka mwezi Oktoba 2016.

Mwaiteleke amesikitishwa na Kitendo cha Mkandarasi huyo kutokamilisha kazi ya Ujenzi wa daraja wakati malipo ya awali ameshalipwa kwa mujibu wa cheti cha Ukaguzi wa wahandisi na timu ya wataalam na kusisitiza akamilishe Ujenzi huo ndani ya siku 14 ili Wananchi waanze kunufaika na huduma bora ya usafiri na kuondoa hofu iliyopo kwa wananchi wanaopita kwa kutumia Daraja la awali la Zamani ambalo kitaalamu halina uimara na uhakika wa kupitika wakati wa masika na mvua kubwa.

Kwa upande wake Mhandisi wa Ujenzi Jacob Uswege kutoka Idara ya ujenzi aliyeambatana na Timu ya Mkurugenzi Mtendaji katika Ukaguzi huo alisema kwamba kazi ya ujenzi wa daraja hilo utagharimu tsh, 164,235,000/= iliyotolewa na kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi wa Mkandarasi Kampuni ya Nella Construction co. Ltd wa Shinyanga na alitakiwa kukamilisha ujenzi katika kipindi kisichozidi muda wa miezi 4 kuanzia Julai hadi Septemba 2016 ambapo kazi hiyo ilitakiwa kukamilika mapema mwaka 2016 lakini kutokana na sababu mbalimbali za kuchelewa kwa vifaa na fedha aliomba kuongezewa muda hadi mwezi Novemba 2016.Halmashauri kupitia Idara ya ujenzi imeendelea kumsisitiza Mkandarasi huyo lakini maendeleo na mwitikio wake ni mdogo na badala yake amekuwa anaomba kuongezewa muda kila hatua ya utekelezaji na kwa mujibu wa mkataba alipaswa kukabidhi daraja hilo mwezi Oktoba 2016.Mkurugenzi Mtendaji Mwaiteleke ameitaka Idara ya Ujenzi kumsimamia Mk