Mama moja wa kijiji cha Lulwangwa halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni amepoteza maisha kwa kutokwa na damu nyingi baada ya yeye na mume wake kuamua kwenda kujifungulia kwenye duka la dawa ambalo halikusajiliwa na aliyetoa huduma hiyo hana ujuzi wa kuzalisha.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kaimu mganga wa halmashauri ya Itigi Daktari Zuberi Hamisi Abdalah amesema pamoja na kwamba uchunguzi bado unaendelea ,lakini mama aliyefariki ametambulika kwa jina la Helena Maduhu aliyekwenda kwenye duka la dawa kwa ajili ya kujifungua baada ya kuambiwa na muuguzi wa zahanati ya Itagata aende hospitali ya Itigi baada ya wao kushindwa.
Akieleza mume wa marehemu bwana bahame kanuda amesema yeye baada ya kuambiwa ampeleke mke wake katika hospita kubwa alikutana na bwana shingu hengwe ambaye ana duka la dawa na kumwomba kumsaidia kumzalisha mkewe .
Bwana Shingu Hengwe anayedaiwa kumzalisha mama huyo katika duka lake la dawa,baada ya mzazi kufariki aliamua kumsafirisha marehemu na pikipiki wakiwa na mumewake kumpeleka kijijini kwao, pikipiki ikaisha mafuta na yeye alitoweka na kutafutwa zaidi ya saa nne kabla ya kukamatwa.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Itigi ambaye aliamua kusimamia shwala hilo ilimlazimu kutuma watu umbali wa zaidi ya kilomita kumina tano ambapo marehemu alipo jifungulia kwenye duka la dawa na kukukuta mtoto aliyezaliwa akiwa mzima kafungiwa ndani ya nyumba akilia huku wenye nyumba hawapo.