F Rais Donald Trump ameliamuru shirika la EPA nchini humo kusitisha kwa muda kandarasi zote | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Rais Donald Trump ameliamuru shirika la EPA nchini humo kusitisha kwa muda kandarasi zote

Rais wa Marekani Donald Trump ameliamuru shirika la ulinzi wa mazingira EPA nchini humo kusitisha kwa muda kandarasi zote pamoja na kuacha kufanya mawasiliano na vyombo vya habari.

Shirika hilo hutoa na kusimamia ruzuku za mabilioni ya dola kila mwaka, ikiwa ni pamoja na viwango vya mazingira, usafishaji na utafiti.
Haijabainika wazi kama kanuni hiyo mpya itaihusu mikataba ya sasa au itakayosainiwa katika siku za usoni.

Maagizo hayo kwa shirika hilo yamekuja baada ya Trump kutoa amri ya rais inayopiga marufuku kwa muda serikali kuwaajiri wafanyakazi, isipokuwa jeshini.
Wakati huo huo Rais alitarajiwa kutia saini amri ya kuweka masharti kuhusu wahamiaji wanaoingia nchini humo ambapo kwa kuanzia ataanza kuimarisha usalama katika mipaka ya nchi hiyo na Mexico.