Maeneo yote yaliyounganishwa kwenye mfumo wa taifa wa kusambaza umeme Tanzania asubuhi yameathiriwa na kukatika kwa ghafla kwa umeme.
Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania limesema tatizo hilo limesababishwa na hitilafu katika mtambo wa kupooza na kusambaza umeme eneo la Ubungo, Dar es Salaam.
Umeme ulikatika mwendo wa saa kumi na mbili unusu asubuhi.
Kaimu meneja uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji amenukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema wataalam wanaendelea kushughulikia tatizo hilo.
"Tatizo hili limetokea leo saa 12:32 asubuhi katika mtambo wa kilovolti 220 ambao ni wa kupoozea na kusambaza umeme uliopo Ubungo lakini kwa kuwa wataalam wameshagundua," Muhaji ameambia Mwananchi.