Takriban wafungwa 152 wameripotiwa kutoroka jela iliyopo katika jimbo la Sao Paulo nchini Brazil.
Maafisa wamefahamisha kuwa kumekuwa na maandamano ya ghasia the mara kwa mara katika jela iliyopo mjini Bauru .
Maandamano hayo yamesabisha wafungwa kupata fursa ya kutoroka .
Hata hivyo operesheni iliyofanywa na askari ya kuwatafuta waliotoroka ilipelekea kupatikana kwa wafungwa 90 , bado askari wanaendelea kuwatafuta wafungwa wengine 62 waliotoroka .
Maafisa wa usalama pia walifahamisha kuwa wafungwa walianzisha moto katika majengo 3 ya gereza hilo.
Huku tukiwa katika mwanzo wa mwaka mpya, nchini zaidi ya wafungwa 100 wamefariki huku wengine zaidi ya 200 wakitoroka .