F BOT kushirikiana na wataalam wa mataifa mbalimbali kudhibiti wizi mitandaoni. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

BOT kushirikiana na wataalam wa mataifa mbalimbali kudhibiti wizi mitandaoni.

Watalaam wa Benk kuu ya Tanzania (BOT) wameanza kushirikiana wataalam kutoka  mataifa mbalimbali kukabiliana na tatizo la wizi kupitia mitandao linaloendelea kutishia usalama wa fedha  katika nchi mbalimbali.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Bank kuu ya Tanzania Bw Rashid Rashid amesema  wameshaanza mjadala na watalaam hao wakiwemo kutoka nchi za SADC juu ya namna ya kulikabili tatizo hili.

Wakizungumzia tatizo hilo jijini Arusha watalam hao akiwemo Mwenyekiti wa maswala ya TEHAMA kutoka nchi ya Msumbiji Bw Alindo Lombe amesema benk kuu za nchi husika zina nafasi kibwa ya kusaidia katika kupambana na wizi wa mitandao.