Rais wa Marekani Donald Trump anajiandaa kuwafanyia mahojiano wale wanaotarajiwa kuchukua wadhifa wa mshauri wa masuala ya usalama wa Marekani, kufuatia kujiuzulu kwa Michael Flynn.
Wale ambao wanatarajiwa kuhojiwa ni pamoja na balozi wa zamani wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa John Bolton na aliye sasa kaimu mshauri Keith Kellogg.
Majemedari wengine wawili ni H.R McMaster na Robert Caslen, pia wamo katika orodha hiyo.
Michael Flynn alijiuzulu Jumatatu ya juma lililopita, kutokana na utata kuhusiana na vikwazo vya Marekani kwa Moscow uliomzingira baada ya kukutana na balozi wa Urusi jijini Washington.