Wakati mshambuliaji wa sasa wa Manchester United Zlatan Ibrahimovich alipokuwa Barcelona,hakuwa katika kiwango kizuri kama alivyokuwa PSG au Inter Millan.Kadabra alihangaika sana Barca kabla ya kuamua kurejea Italia kukipiga Italia katika timu ya Ac Millan.
Zlatan wakati anajiunga na Barcelona alisaini mkataba wa miaka mitano,lakini alitumia miezi 12 tu kabla ya kuondoka.Katika miezi hiyo 12 Kadabra alifanikiwa kuifungia Barcelona jumla ya magoli 21 katika mashindano yote,lakini pamoja na yote hayo aliamua kuondoka Barcelona ambayo kipindi hicho alizungukwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu akiwemo Lioneil Messi na Thiery Henry.
Sasa siri ya Kadabra kutodumu na kutoonesha makali yake akiwa na Barcelona imefahamika.Inaaminika Ibrahimovich hakuwa na uhusiano mzuri na baadhi ya watu katika timu ya Barcelona akiwemo Lioneil Messi lakini pia uhusiano wake na kocha Pep Gurdiola nao ulikuwa chanzo cha Zltan kuondoka.
Katika uchezaji Messi alihitaji nafasi/eneo kubwa la kucheza jambo ambalo pia Zlatan alilitaka.Meneja masoko wa zamani wa Barcelona Marc Ingla anasema msuguano wa chinichini kati ya Zlatan Ibrahimovich na Lioneil Messi ulikuwa unamfanya Zlatan kufanya kile atakacho uwanjani hali iliyopelekea kuondoka kwake.
“Kwa nini hakufanikiwa Barcelona?Zlatan ni hatari ni mashine lakini pembeni yake kulikuwa na kamashine kadoogo (Messi),naamini kulikuwa na msuguano kati ya mashine hizo” alisema Ingla ambae kwa sasa anafanya kazi na timu ya Lille ya nchini Ufaransa.Zlatan sasa yuko Uingereza huku akifunga tu karibu kila wiki na Messi nae akiendelea kung’ara La Liga.