F OCCID wa polisi Kibiti auwawa na majambazi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

OCCID wa polisi Kibiti auwawa na majambazi

Kibiti. Watu watatu akiwamo OCCID wa Wilaya ya Kibiti, Peter Kubezya wamefariki dunia kwa kupigwa risasi na watu wadhaniwa kuwa ni  majambazi katika Kijiji cha Jaribu wilayani hapa.

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Gullamuhusein Kifu amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema watu sita  wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za moto walikivamia kituo change Wiley's cha kukusanyia ushuru kilichopo kijijini hapo.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa mauaji hayo yametokea usiku wa kuamkia leo Jumatano ambapo  watu hao wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa na bunduki walivamia kuzuizi cha maliasili kilichopo kijijini hapo  na kukichoma moto kabla ya majibizano ya risasi na polisi wakiokuwa doria kwenye eneo hilo.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Misheni ya Mchukwi, Zakaria Lukeba amethibisha kufikishwa kwa mwili  Kubezya ukiwa na jeraha la risasi tumboni pamoja na maiti mbili ambazo hazijajulikana majina.