F Ukata kuchelewesha utoaji wa haki | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Ukata kuchelewesha utoaji wa haki

Bukoba.  Ukata katika Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba umesababisha majaji kutoendeleza vikao vya kusikiliza mashauri 24 ya kesi za mauaji, hali itakayosababisha haki kutokutolewa kwa wakati.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Salvatory Bongole akizungumza wakati wa kilele cha siku ya sheria nchini, alisema hadi Desemba mwaka jana hakuna kesi iliyokuwa imezidi miezi sita katika mahakama zote za mwanzo.

Alisema wamejitahidi kumaliza mashauri mengi kwa wakati pamoja na kupunguza malalamiko,  huku kesi 81 zikizidi mwaka mmoja katika mahakama za wilaya kwa kuwa korti hizo hazikuwa na uwezo nazo.

Oktoba 27 mwaka jana katika kesi ya jinai namba 67/2015, Mahakama Kuu chini ya Jaji Firmini Matogolo ilitoa uamuzi baada ya  miaka minane kwa  kuwatia hatiani wanandoa Lameck Bazil na Pancras Minago kwa mauaji ya mlemavu wa ngozi, Magdalena  Andrea yaliyotokea mwaka 2008 wilayani Biharamulo mkoani Kagera.