Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba pamoja na Mbunge wa jimbo la Segerea Mh. Bonnah Klauwa wakiskiliza kero mbalimbali zinazotolewa ana Wananchi wakati Mh. Waziri alipofanya ziara katika kata ya Vingunguti kukagua athari mbalimbali za mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amewataka wachimbaji mchanga na walimaji wa bustani katika bonde la mto msimbazi katika kata vingunguti iliyopo katika Manispaa ya Ilala, kuondoka mara moja na kuacha shughuli hizo.
Ameyasema hayo alipokua katika ziara ya siku moja ya kutembelea kata ya Vingunguti na kujionea athari mbalimbali za kimazingira katika kata hiyo.
Wakiongea mbele ya Waziri Makamba, Wananchi wamelalamika kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo bonde hilo kuzidi kumong'onyoka na kusogelea makazi ya watu pamoja na eneo la makaburi.
Hivyo basi kusababisha nyumba zao kuanguka na makaburi kumong'onyoka hali amabayo inahatrisha maisha yao na kuwafanya kuishi kwa hofu.
Akijibu kero hiyo Waziri Makamba aliwaambia kuwa atayafanyia kazi maombi yao na atakaa na viongozi wa Manispaa na wa Ofisi yake ili kupata suluhu ya matatizo yao.
Pamoja na hayo alisema kuwa kwa hatua za awali anawataka wachimbaji na wakulima wa bustani kuacha mara moja shughuli hizo wanazofanya katika maeneno ya bonde hilo.