F Asilimia 25% ya wastaafu wanapoteza maisha | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Asilimia 25% ya wastaafu wanapoteza maisha



Asilimia 25% ya wastaafu wa serikali nchini,wanapoteza maisha mapema kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kushindwa kujiandaa kimaisha mapema huku baadhi yao wakiongeza idadi ya wake na kusababisha kuathirika kimaendeleo.

Akizungumza na watumishi wa serikali kutoka mikoa mbali mbali hapa nchini waliobakisha muda mchache kabla ya kustaafu ,Mkurugenzi wa Chuo cha utumishi wa umma kampasi ya Tanga,Hassanal Isaya amesema utafiti walioufanya katika mikoa mbali mbali nchini umeonesha kuwa baadhi ya watumishi wanashindwa kujiandaa na maisha ya kujitegemea kwa sababu ya mazoea ya kazi.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Chuo cha utumishi wa umma nchini Dr,Henry Mambo amesema serikali imekuwa ikitoa elimu kwa watumishi wake ili waweze kujiandaa na maisha baada ya kustaafu hivyo amewashauri watumishi kuacha anasa na badala yake wajikite kuwekeza katika sekta ya elimu kwa watoto wao.

Kufuatia hatua hiyo,baadhi ya watumishi wa serikali wanaotarajiwa kustaafu wameishukuru serikali kwa kuwakumbusha na suala la kujiandaa baada ya kustaafu na baadhi yao wameanza mchakato wa kujitegemea ili kuepukana na maisha ya kutangatanga katika jamii.





Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote, Basi hii Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ... 

Chakufanya ni Kubofya Link hapo chini na Ufate Maelekezo ya Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..

Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako... USIWE NA WASIWASI HUDUMA HII NI SALAMA KABISA..