Kamanda Mpinga Afunga Kampeni ya ‘Abiria Paza Sauti’ Ubungo Dar

Kamanda Mpinga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madereva walipatiwa vyeti kutokana na uendeshaji bora wakiwa barabarani.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP), Mohamed Mpinga amewaasa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali na abiria kutoa taarifa kwa wanaokiuka sheria hizo kwa kutoa taarifa kwa wakati.

Hayo ameyasema leo wakati wa kufunga Kampeni ya ‘Paza Sauti’ iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania katika Kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo Dar.

Akifafanua alisema, kila mtu anawajibu wa kutoa taarifa dhidi ya dereva anayehatarisha maisha katika vyombo vya usafiri.
“Dereva kutokujua sheria za usalama barabarani isiwe kigezo cha kuvunja sheria zilizowekwa kwani waathirika wakubwa wa ajali ni Watanzania ambao ndiyo nguvu kazi ya kesho,”alisema Kamanda Mpinga.

Aidha aliendelea kufafanua kuwa, kampeni hiyo ilileta matokeo chanya ambayo yameonyesha kupungua kwa ajali na hata kampeni itakayokuja tena iungwe mkono.

Naye Mwenyekiti wa Kampeni ya ‘Paza Sauti’ iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA, John Beniel amesema wao kwa kupitia abiria waliweza kupata taarifa mbalimbali na kuzifanyia kazi ambazo walifanyia kazi kupitia vyombo vinavyohusika vya usalama barabarani kwa madereva waliovunja sheria.

Katika kufunga kampeni hiyo, mabalozi wa usalama barabarani kutoka taasisi ya RSA (Road Safety Ambassadors) pia wamekabidhi kwa baadhi ya maderva vyeti na mabati 15 kwa kila dereva ambaye alipigiwa kura na madereva wenzake kwa kuonesha mchango wake akiwa barabarani kwa kuendesha vizuri.