Dar es Salaam. Siku moja baada ya Mbunge wa Kilombero (Chadema) Peter Lijualikali kuachiwa huru na mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam, ametoa ya moyoni na kusema kuwa alichofanyiwa ni uonevu.
Ameyasema hayo leo baada ya Waziri Mkuu Mstaafu, na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye, kukamilisha taratibu za kumtoa gerezani.
Lijualikali amefutiwa mashtaka yake jana na mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam baada ya kukaa jela kwa zaidi ya siku 70 akituhumiwa kufanya vurugu katika uchaguzi wa mwaka 2015. Katika hukumu hiyo, Lijualikali alihukumiwa bila kupewa masharti ya faini.