F Makada wa CHADEMA washinda kesi ya operesheni UKUTA | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Makada wa CHADEMA washinda kesi ya operesheni UKUTA

.Na.Ahmad Mmow.
Mahakama ya mkoa wa Lindi,leo imewachia huru makada watatu wa CHADEMA waliokuwa wanakabiliwa na shitaka la kushiwishi kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usiohalali,ambalo nikinyume cha sheria kwamujibu wa kifungu cha 74(1) na (2) sheria ya adhabu sura ya 16.Akisoma hukumu ya kesi hiyo ya jinai namba 88/2016,hakimu mkazi mwandamizi mfawidhi wa mahakama hiyo,

Geofrey Mhini,alisema mahakama hiyo baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka uliokuwa unaongozwa na wakili wa serikaliJuma Maige na waupande wa utetezi uliokuwa unaongozwa na wakili wa kujitegemea,

Deusdedit Kamalamo iliwaona washitakiwa Hamis Namangaya aliyekuwa mwenyekiti wa  CHADEMA wa kanda ya kusini,Filbert Ngatunga(mratibu wa kanda) na Zeud Abdallah(ofisa toka makao makuu) hawakuwa na hatia.Hivyo iliamua kuwa achia huru.Hakimu Maige alisema mahakama hiyo haikuona mahusiano yoyote baina ya mafunzo na yaliyotajwa na upande wa mashitaka kuwa yalikuwa na lengo la kuwaandaa washiriki kufanya mkusanyiko,mikutano na maandamano yaliyotarajiwa kufanya Septemba Mosi mwaka jana,yaliyojulikana kama opesheni
UKUTA.

Alisema upande wa mashitaka ulishindwa kupeleka ushahidi usio na shaka ulioonesha mafunzo hayo yalikuwa na lengo lililotajwa na upande wa mashitaka."Mahakama imeridhika kuwa yalifanyika mafunzo hayo ambayo yaliwashirikisha viongozi wa wilaya,milkoa wa Lindi na madiwani wanaotokana na chama hicho.Bali ubishi nikwamba mafunzo hayo yalilenga kuwashawishi washiriki watende kosa la kufanya maandamano na mikutano ya hadharani Septemba mosi?Ilibain hakuna muunganiko na uhusiano wowote na shitaka lililoletwa na upande wa mashitaka ," alisema Mhini.

Alibainisha kwamba kukosekana ushahidi madhubuti dhidi ya viongozi hao,mahakama kwa kutumia kifungu cha 235 sura ya 20 ya sheria adhabu ya mwaka 2005 nakufanyiwa marekebisho mwaka 2012 iliwaachia huru.

Awali wakili Maige aliambia mahakama hiyo tarehe 13 Agosti mwaka jana wakiwa katika ukumbi wa mtakatifu Andrea Kagwa uliopo manispaa ya Lindi walitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo na hamasa washiriki waliokuwa katika ukumbi huo waweze kuwa na hamasa ya kushiriki maandama na kufanya mikutano iliyopigwa marufuku na serikali,iliyotambulika kwa jina la opereshkuwatumikiHata hivyo viongozi hao waliokuwa wanatetewa na wakili Deusdedit Kamalamo,walipinga na kukana shitaka hilo.Badala yake walisema mafunzo hayo yalikuwa ya kawaida yalikuwayo kuwa na lengo la kuwqjengea uwezo wa uongozi ili kuwatumiki kwa ufanisi wananchi na wanachama wao.