Nchi hii imeondolewa kwenye Orodha ya Trump


Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini amri mpya ya kupiga marufuku wahamiaji kutoka nchi sita za kiislamu kuingia Marekani, katika amri iliyotolewa awali na kuzuiwa na mahakama ilizitaja nchi saba, lakini sasa Iraq imeondolewa kwenye orodha ya sasa.

Serikali ya Marekani inasema nchi zilizoorodheshwa zinafadhili ugaidi au zimeshindwa kupambana na magaidi wanayofanya shughuli zao ndani ya nchi zao.

Wakosoaji wa mpango huu wa Trump wamesema kuwa hatua hii inakwenda kinyume na Katiba kwa kuwa msingi wake umeegemea kwenye ubaguzi wa kidini.

Nihad Awad kutoka Baraza la Kiislam nchini Marekani linalotafuta kujenga mtazamo chanya wa dini ya kiislamu nchini humo, amesema watapambana dhidi ya Amri hiyo

Naye Kaimu mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za wamarekani " American Civil Liberties Union "Lee Gelernt amesisitiza kuwa amri hii haiiweki Marekani mahala salama

''hatufikiri kuwa amri hii ni muhimu kwa usalama wa taifa,lakini si sisi tunaosema hivyo , ni wataalam wa masuala ya usalama na wanadiplomasia wanaoheshimika kutoka uongozi wa Democratic na Republican ambao awali walichukua hatua za kufungua shauri mahakamani wakipinga amri hii wakisema haita tufanya kuwa salama, zaidi ya yote tunaona nakala iliyovuja kutoka idara ya mambo ya ndani, maafisa wakisema kuwa mpango huu hautasaidia usalama wa taifa letu''

Nchi zilizoorodheshwa kwenye amri hii mpya ya Donald Trump ni Iran, Sudan, Syria, Libya, Somalia na Yemen.Mwanasheria mkuu wa Serikali Jeff Sessions, ameviambia vyombo vya habari kuwa nchi tatu kati ya zilizotajwa zinafadhili ugaidi na nyingine tatu zimeshindwa kabisa kupambana na wanamgambo kama vile Islamic State na Al Qaeda.




Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote, Basi hii Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ... 

Chakufanya ni Kubofya Link hapo chini na Ufate Maelekezo ya Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..

Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako... USIWE NA WASIWASI HUDUMA HII NI SALAMA KABISA..