ZAIDI ya vijiji 7,000 kati ya vijiji 12,000 vilivyopo nchini vinatarajiwa kunufaika na nishati ya umeme

ZAIDI ya vijiji 7,000 kati ya vijiji 12,000 vilivyopo nchini vinatarajiwa kunufaika na nishati ya umeme utakaosambazwa na Wakala wa usambazaji umeme vijijini (REA) awamu ya tatu ifikapo mwaka 2019.

PROF.MUHONGO ameyasema hayo katika Kijiji cha Mkwese,wilayani Manyoni,Mkoani Singida alipokuwa akizindua mradi kabambe wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu uliofanyika katika Mkoa wa Singida.

AMESEMA Waziri huyo kwamba kwamba katika kipindi cha miaka miwili miradi hiyo ya awamu ya tatu itakuwa imekamilika na kwamba ili miradi hiyo iweze kukamilika kunahitaji fedha zinazotokana na vyanzo viwili vya fedha vinavyotegemewa ambavyo ni asilimia 50 inayotoka katika vyanzo vya ndani na asilimia nyingine hamsini inatokana na misaada kutoka nchi za nje wakiwemo walipa kodi wa Norway na Sweden.

NAYE Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, MHANDISI GISSIMA NYAMO-HANGA amesema katika mradi wa umeme awamu ya tatu vijiji 185 ambavyo kati ya hivyo,150 vitakuwa katika mpango wa kawaida wa kuongeza wigo wa umeme vijijini na vijiji 35 ni vile vinavyopatiwa umeme kwa kuwa jirani na Mkuza mkubwa wa umeme unaosafirisha umeme kutoka Iringa kupitia Dodoma,Singida,Tabora hadi Shinyanga.

Kwa upande wao Balozi wa Sweden Nchini Tanzania, KATARINA RAANGNITLY amesisitiza kwamba matumizi ya nishati ya umeme katika viwanda vidogo nchini yataongeza thamani ya mazao pamoja na kuzalisha kazi kwa ajili ya jamii wakati Balozi Norway Nchini Tanzania,HAMME HANIE KAARSTAD amesema upatikanaji wa umeme unafungua fursa kwenye uzalishaji kwenye viwanda vidogo vidogo pamoja na maendeleo mengine ya wananchi.