Zitto akerwa kampuni kubwa kutolipa kodi

Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema Serikali inapaswa kujikita katika kuzishughulikia kampuni kubwa ambazo hazilipi kodi badala ya kushughulika na wafanyabiashara wadogo wadogo.

Zitto amesema hayo  kwenye mkutano huo mkuu wa kidemokrasia wa kujadili miaka 50 ya Azimio la Arusha juzi.

Amesema kuna idadi kubwa ya kampuni za uwekezaji ambazo zinakwepa kulipa kodi hivyo kuliingizia hasara Taifa, lakini hazichukuliwi hatua.

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema anasikitishwa na vitendo vya watu waliokwenda kumtembelea gerezani kuitwa wasaliti.

“Kama ni suala la usaliti, basi Zitto Kabwe awe msaliti namba moja kwa kuwa alikuwa anakuja mara kwa mara na kupambana nitoke gerezani,” amesema.