F Kombora jingine la Korea Kaskazini lafeli majaribio | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kombora jingine la Korea Kaskazini lafeli majaribio

Rais wa Marekani Donald Trump ameishtumu Korea kaskazini kwamba imeikosea heshima China, mshirika wake mkuu, kwa kufyatua kombora la tatu katika kipindi cha mwezi mmoja.

Kwenye ujumbe wa Twitter, bwana Trump amemsifu rais wa Uchina, Xi Jinping.
Maafisa wa Marekani na Korea Kusini wanasema jaribio hilo lilitibuka, kwani kombora hilo lilianguka punde tu baada ya kupaa angani.

katika mkutano wa baraza la usalama la umoja wa mataifa, Rex Tillerson, ameonya kwamba huenda kukaibuka majanga mabaya sana iwapo miradi ya Kim Jong Un ya kutengeneza zana za kinyuklia na makombora ya masafa marefu hiatositishwa.

Maafisa wa Marekani wanasema kombora hilo lilipaa angani kwa sekunde kadhaa kabla ya kuanguka.

Hii ni ishara kwamba Korea Kaskazini haina ujuzi wa kutosha kiteknolojia, ama pia huenda ikawa Marekani imepata mbinu ya kuingiilia mifumo yake ya teknolojia.

Maafisa wakuu wa Korea kusini na Japan wamekashifu vikali majaribio ya hayo.
Msemaji wa wizara ya mabo ya nje wa korea kusini anasema Pyongyang inacheza na moto.

Msemaji wa serikali ya Japan anasema jaribio hilo ni kinyume na mapendekezo ya umoja wa mataifa.

Gazeti la the Newyork Times, linasema kwamba Marekani imeweka virusi kwenye kompyuta za kijeshi za Korea kaskazini, japo madai hayo yanatiliwa shaka.

Haya yanajiri siku moja baada ya Marekani kuweka wazi mikakati yake ya kukabiliana na Korea kaskazini ikiwemo kuanza vita dhidi ya taifa hilo, na kutoa ahadi kwamba serikali ya Kim Jong un haitapinduliwa iwapo atasimamisha miradi yake ya kutengeneza zana za nyuklia na makombora ya masfa marefu.

Korea Kaskazini imefyatua makombora 75 tangu rais Kim Jong un aanze kutawala.