mashamba ya bangi yazidi kufichuliwa

Takriban hekari kumi za mashamba ya bangi zimebainika katika wilaya ya Rungwe Mbeya ambapo hekari saba na nusu zimeteketezwa.

Zoezi hili ambalo limefanyika chini ya kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya ikiongozwa na mwenyekiti wake Julius Challya, wamebaini hekari kumi za bangi ambapo hekari saba na nusu zimevunwa na kuteketezwa Mkuu wa Wilaya hiyo anasema zoezi hili ni endelevu ambapo amewataka wananachi kuacha mara moja ulimaji wa bangi.

Afisa Mtendaji wa kata ya Isongole Esau Chonya yalipobainika mashamba haya anasema wamebaini uwepo wa mashamba haya baada ya kufanya ukaguzi wa misitu na wakala wa huduma za misitu TFS.

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Julius Challya anasema zoezi hili ni endelevu, na kwamba kamati ya ulinzi na usalama itaendelea na ukaguzi wa milima na misitu yote baada ya kubaini bangi hiyo kulimwa katikati ya misitu.