MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe amtuhumu Rais John Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusika kwa alichodai kuwa ni kukeukwa kwa taratibu za uchaguzi.
Mbowe ameongea hayo jana usiku mara baada ya kutoka kwenye ukumbi wa bunge ambapo amedai kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Rais Magufuli kuhusika kwenye mchakato wa kuyakataa majin ya wagombea wa Chadema.
Mbowe amesema kuwa, wao hawatakubaliana na hilo kwa sababu Spika wa Bunge amekiuka kanuni za bunge, na uchaguzi wote ulikuwa wa kasoro.
Wagombea waliopendekezwa na Chadema Wenje Na Masha kupigiwa kura za hapana katika kuwania kuiwakilisha Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki
Majina ya wagombea na matokeo
KUNDI A: WANAWAKE
1. Ndg. Happiness Elias LUGIKO - KE - CCM - KURA 196
2. Ndg. Fancy Haji NKUHI - KE - CCM - KURA 197
3. Ndg. Happiness Ngoti MGALULA - KE - CCM - KURA 125
4. Ndg. Zainabu Rashidi Mfaume KAWAWA - KE - CCM - KURA 137
KUNDI B: ZANZIBAR
1. Ndg. Abdullah Hasnu MAKAME ME CCM - KURA 254
2. Ndg. Maryam Ussi YAHYA KE CCM - KURA 195
3. Ndg. Mohamed Yusuf NUH ME CCM - KURA 65
4. Ndg. Rabia Hamid MOHAMEDI KE CCM - KURA 142
KUNDI C: VYAMA VYA UPINZANI
CHADEMA
1. Ndg. Ezekia Dibogo WENJE - ME - CHADEMA - KURA ZA NDIYO 124 HAPANA 174
2. Ndg. Lawrence Kego MASHA - ME - CHADEMA - KURA ZA NDIO 126 HAPANA 198
CUF
1. Ndg. Habibu Mohamed MNYAA - ME - CUF KURA 188
2. Ndg. Sonia Jumaa MAGOGO - KE - CUF KURA 06
3. Ndg. Thomas D.C MALIMA - ME - CUF- ALIJIONDOA
4. Ndg. Twaha Issa TASLIMA - ME - CUF KURA 140
KUNDI D: TANZANIA BARA
1.Ndg. Adam Omai KIMBISA - ME - CCM 266
2. Ndg. Anamringi Issay MACHA - ME - CCM 23
3. Ndg. Charles Makongoro NYERERE - ME - CCM 81
4. Dkt. Ngwaru Jumanne MAGHEMBE - ME - CCM 287
Wabunge saba ndio wamechaguliwa na nafasi mbili za CHADEMA bado zipo wazi.
WALIOSHINDA NI;
1. Fancy Haji Nkuhi
2. Happiness Elias Lugiko
3. Abdallah Hasnu Makame
4. Maryam Ussi Yahya
5. Habibu Mohamed Mnyaa
6. Ngwaru Jumanne Magembe
7. Adam Omary Kimbisa