F Nikki Mbishi: nataka kuwakomboa wanawake | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Nikki Mbishi: nataka kuwakomboa wanawake

Rapa kutoka Tanzania anayefanya vizuri na ngoma ‘Sam Magoli’ Nikki Mbishi ametangaza ujio wake mpya wa kutaka kuwarekebisha wadada ambao wanatumia pesa nyingi kurekebisha miili pamoja na ngozi.

Rapa kutoka Tanzania anayefanya vizuri na ngoma ‘Sam Magoli’ Nikki Mbishi ametangaza ujio wake mpya wa kutaka kuwarekebisha wadada ambao wanatumia pesa nyingi kurekebisha miili pamoja na ngozi.

Kupitia ukurasa wake Instagram Nikki Mbishi ametoa ujumbe huo kwa kuweka kionjo kuwa anayo zawadi ya wimbo utakaokwenda kwa jina la 'Dada pumzisha mwili wako' maalumu kwa akina dada wanaotumia muda na pesa zao katika kujitengeneza vile wanavyotaka wawe.

Aidha Nikki amefafanua kuwa lengo la kuachia wimbo huo ni kutoa elimu zaidi kwa matumizi ya madawa na vipodozi vyenye madhara madogo na makubwa katika miili ya watumiaji.

"Baada ya 'IamSorryJK na Sam_Magoli' msanii wako bora wa siku zote @nikkimbishi anakuja na kazi mpya iitwayo 'Dada Pumzisha Mwili Wako'.

Wimbo ambao ni dedication kwa wadada wote wanaodhani uzuri unauzwa dukani kiasi cha kutumia vipodozi na dawa za kubadili maumbo na sura zao. Lengo la wimbo ni kukumbusha madhara ya kutumia vipodozi kupita kiasi kitu ambacho kimekuwa kikihatarisha afya ya ngozi na hata uzazi kwa ujumla pamoja na mambo mengine ya kitaalamu zaidi"- Nikki Mbishi.

Nikki ambaye ni miongoni mwa marapa ambao wamewahi kuingia katika orodha za wasanii ambao nyimbo zao zimewahi kufungiwa kwa kuwa na mashairi yasiyo na maadili, ametaja tarehe rasmi ya ujio wa ngoma hiyo kuwa ni 28  April 2017.