F TMA: Mvua kubwa kunyesha usiku wa leo Jumatatu hadi Jumatano | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

TMA: Mvua kubwa kunyesha usiku wa leo Jumatatu hadi Jumatano

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari  kwa Watanzania  juu ya kuendelea kunyesha kwa mvua kubwa kuanzia leo Jumatatu hadi  Jumatano.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyoitoa leo (Jumatatu), mamlaka hiyo imesema kutakuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24.

Mamlaka hiyo imesema mikoa itakayoathirika ni Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

“Mvua hii yenye wastani wa asilimia 60, inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua nchini,” imesema taarifa hiyo.

Kutokana na hali hiyo, mamlaka imewataka wakazi mikoa hiyo kuchukua hatua stahiki.