F Mapambano dhidi ya wahamiaji haramu Rukwa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mapambano dhidi ya wahamiaji haramu Rukwa

WIMBI la wahamiaji haramu kutoka nchi jirani ya DRC limedaiwa kuwa kikwazo cha utoaji wa huduma kama chanjo, magonjwa ya mlipuko na vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi katika mwambao wa Ziwa Tanganyika katika wilaya za Nkasi na Kalambo mkoani Rukwa na kuwalazimu madiwani wa wilaya ya Nkasi kuiomba Serikali kushughulikia haraka suala hilo.

Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Nkasi limeezwa kuwa katika kata za mwambao wa Ziwa Tanganyika kumekuwa na wimbi kubwa la wahamiaji haramu wengi wao wakitokea nchi jirani ya DRC.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Nkasi na mkuu wa wilaya amekiri kuwepo kwa wahamiaji haramu katika wilaya yake.