"Idadi ya watalii wanaoingia nchini inapatikanaje? Hili swali ambalo wengi huwa hatujiulizi tunapozungumzia utalii na idadi ya watalii. Kila mtu anayeingia kwenye mpaka wa tanzania na kujaza fomu ya uhamiaji ( entry form ) anaingizwa kwenye kanzidata ya watalii.
Wale wanaokwenda kwenye hifadhi za taifa pia wanaweza kuhesabiwa zaidi ya mara moja. Mfano unapoingia Tarangire unahesabiwa. Ukienda Manyara unahesabiwa pia. Ukienda Serengeti unahesabiwa tena. Ukimalizia Gombe National Park unahesabiwa tena.
Nadhani Nchi inahitaji namna mpya ya kuhesabu watalii wanaoingia nchini ili kuwa na takwimu za uhakika. Tunaweza kutumia teknolojia kujibu changamoto hii"- Ameandika Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook