F Ofiisa Usalama Jela miaka 20 kwa kukutwa na Mafuta ya Simba | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Ofiisa Usalama Jela miaka 20 kwa kukutwa na Mafuta ya Simba


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka 20 jela Ofisa Usalama, Saidi Rajabu Saidi (36) baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na mafuta ya Simba yenye thamani ya Sh10,711,400 bila kibali.

Hukumu hiyo imetolewa leo (Jumatano) na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri  mara baada ya mashahidi wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao na washtakiwa kujitetea.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kufanya kosa hilo kinyume na kifungu 86(1)(2)(c)(ii) ya sheria ya wanyamapori namba 5 ya 2009.

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, Wakili wa Serikali, Adolf Mkini aliomba mahakama itoe adhabu kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia na nia ya kutenda makosa kama hayo.

Kwa upande wa mshtakiwa aliiomba mahakama imuachie huru kwa sababu ana watoto watano na familia inayomtegemea na yeye ndio mpangaji wa nyumba alisisitiza kuomba aachiwe huru na hata rudia tena.

Katika kesi hiyo anadaiwa kuwa Februari 8,2016 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) mtuhumiwa alikamatwa akiwa na mafuta hayo ya Simba yenye thamani ya Sh 10,711,400 bila ya kuwa na kibali cha mkurugenzi wa wanyamapori.