New York, Marekani .Mwanamuziki Rihanna alivunja mahusiano yake na mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema kwa sababu ya mapenzi yake kwa Chris Brown.
Wawili hao walitaka kuwa kama Posh na Becks, lakini ndoto ya Benzema kumchumbia Rihanna ilikwama.
Mwaka 2015, kulikuwa na tetesi kuwa nyota hao wawili walikuwa wakikutana mara kwa mara na kufurahi pamoja.
Pamoja na Benzema na Rihanna kutembelea muda mwingi hasa katika mjini ya Hollywood na LA, lakini kulikuwa na kikwanzo kimoja katikati yao… ni mchumba wa zamani wa Rihanna, Chris Brown.
Kwa mujibu wa jarida la Hispania la Don Balon Rosa, sababu kubwa ya uchumba huo ukwama ni mwanamuziki Brown ndiye chanzo Rihanna na Benzema kushindwa kutangaza uchumba wao hadharani.
Mmoja wa marafiki wa karibu wa Benzema alikaririwa na Don Balon akisema: “Rihanna anampenda Karim, akiwa naye anakuwa na furaha sana.
“Lakini alimwambia kwamba hawezi kuumiza moyo wake, kwa sababu penzi lake lipo zaidi Chris Brown.
“Rihanna alisema ni vigumu kuchanganya penzi.”