F Sembe yazidi kupaa Zanzibar | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Sembe yazidi kupaa Zanzibar

MFUMKO wa bei za bidhaa Zanzibar umeongezeka kwa mwezi wa Aprili ikilinganishwa na mwezi wa Machi mwaka huu, unga wa sembe ukiongoza.

Akitoa ripoti ya hali ya mfumuko wa bei visiwani humo, Ofisa wa Mtakwimu Mkuu, Khamis Msham, alisema mfumko wa bei kwa mwezi Aprili umepanda kwa asilimiia 7.1 na mwezi Machi ulikuwa asilimia 6.4.

Alisema bei ya unga wa sembe imepanda kwa asilimia 6.7 kwa mwezi Aprili kwa kilo moja kuuzwa kwa Sh. 2000 kwa mwezi Machi Sh. 1,800.

Alisema pia bei ya ndizi mbichi imeongezeka kutoka asilimia 7.2 mwezi wa Machi hadi kufikia asilimia 7.2 kwa mwezi wa Aprili wakati ndizi mbivu imepanda kwa asilimia 19.1 .

Bidhaa zingine zilizopanda bei ni vinywaji visivyo na kilevi ambavyo kwa mwezi April ilikuwa asilimia 2.9 kwa mwezi mchele wa Mbeya umepanda kwa asilimia 2.6 na sukari 27.1,

Hata hivyo matarajio ya kuongzeka zaidi kwa mfumko wa bei wa bidhaa mbalimbali unatarajiwa kuwa mkubwa kwa mwezi wa Mei wakati waumini wa dini ya Kiislamu wakitarajia kufunga mfungo wa mwezi Ramadhani, mwishoni mwa mwezi huu.

Ofisa Mwandamizi wa Uchumi wa Benki Kuu (BOT), Moto Ngwinganele Lubogi, alisema msukumo wa mfumko wa bei za bidhaa hasa vyakula umesababishwa na uzalishaji mdogo kwa wakulima.

Alisema bei ya unga wa sembe imepanda kutokana na uzalishaji wa mahindi kupungua Tanzania bara, kutokana na maeneo kuchelewa kupata mvua.
Alisema wafanyabiashara wamekuwa wakipandisha bei za bidhaa kutokana na kiwango alichonunua kutoka kwa mkulima.

Hata hivyo, alisema kuwa ili mfumko wa bei za bidhaa hasa chakula uweze kushuka, wananchi wanatakiwa kuongeza uzalishaji wa kilimo na kuacha kulima kilimo cha mazoea cha kutegemea mvua.