F Zitto: Kwasasa namuunga mkono Rais, Mengine tutatofautiana huko mbele | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Zitto: Kwasasa namuunga mkono Rais, Mengine tutatofautiana huko mbele

"Jambo la msingi Sana wakati huu ni kumsaidia Rais kuhakikisha Tanzania inashinda vita ya kurudisha rasilimali za nchi Kwa Nchi yetu. Kwa watu wanaopigania mabadiliko makubwa kwenye sekta ya madini, Rais ametupa fursa. Tuitumie kupigania mabadiliko ya mfumo wa uzalishaji kwenye madini, haki za wafanyakazi wa migodi, masuala ya mazingira na kuzuia upotevu wa mapato. 

Hii ni vita, Hii Ndio tunaita Demokrasia ya Rasilimali kwa muktadha wa uzalendo wa Rasilimali (Resources Nationalism). Kwa sasa masuala mengine nayaweka pembeni, tushirikiane na Rais kufanikisha jambo la nchi yetu. Mengine tutatofautiana huko mbele."- Ameandika Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook leo Mei 25, 2017.