Chama cha ACT-Wazalendo kimelaani kitendo cha Jeshi la Polisi kuwazuia kwa nguvu walemavu waliotaka kwenda kumuona Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Ilala.
Akizungumza na waandishi wa habari leo (Juni 18), Katibu wa Itikadi wa ACT, Ado Shaibu amesema walemavu hao walikusanyika ili kwenda kupeleka malalamiko yao dhidi ya askari wa usalama barabarani kuwakamata na kuwazuia kuingia katikati ya jiji.
"Juni 16, askari polisi waliwavamia, kuwapiga, kuwaswaga na kuwaburuza watu wenye ulemavu," amesema Shaibu.
ACT imemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuomba radhi kwa jumuiya ya watu wenye ulemavu nchini na kuhakikisha vitendo hivyo havirudiwi.