CHAMA Cha Act-Wazalendo Mkoa wa Kagera kimesema kuwa wanasiasa wanaolitumia jina la chama na Kiongozi wa Chama hicho Zitto Kabwe kwa ajenda za Propaganda mbaya wamefeli.
Propaganda hizo ni pamoja na kukihusiha chama hicho na Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja kumtaja na kiongozi kuwa atapewa nafasi kubwa kwenye Serikali ili kukiua chama hicho.
Hayo yamelezwa na Katibu wa Vijana wa Chama hicho Mkoa huo Khalfani Fadhili kupitia ukurasa wake wa mtandao wa picha wa Instergram (@ khalfani_fadhili) ambapo amesema kuwa Chama hicho hakitarudi nyuma na kwamba hawatayumbishwa na Propaganda za wanasiasa wenye nia ovu na chama hicho.
Amesema kuwa baadhi ya kauli za wanasiasa kuwa Zitto Kabwe atafungwa na Mdomo kwa kupewa nafasi ndani ya Serikali kuwa sio za kweli na hazina afya kwenye siasa nchini.
“Zitto sio mmiliki wa ACT wazalendo bali ni mwanachama wa ACT na ni mbunge mwenye dhamana ya chama pia ni kiongozi mkuu katika chama.Hivyo ukikuta mwanasiasa mwenye nia ovu kwa kauli zao za kuwaaminisha watu kuwa Zitto yuko mbioni kupewa Uwaziri ili Act-Wazalendo ife jua huyo ni mwanasiasa aliyefilisika”
Amesema kuwa wapo wanaowamisha watu kuwa Act-Wazalendo ni sehemu ya CCM ilhali chama cha Act kina sera za kulijenga taifa , ujamaa na uzalendo kwa kushirikiana na watanzania wote bila kujali itikadi zao.
“Sikatai kuwa haiwezi kuwa akapewa nafasi nyeti katika serikali hii inayoonyesha kuguswa na viongozi wa ACT.bali nakataa wale wanaolazimisha watu waamini kuwa ACT ni sehemu ya CCM.Yanaongelewa mengi kuwa Mh.Zitto atafungwa mdomo kwa kupewa nafasi ya juu ili anyamaze.hayo ni maneno ya chuki dhidi ya chama chetu kwani hata wao wanazitamani nafasi tulizozipata ACT katika kuilitumikia taifa hili.”