F Hatuna shida ya mafuta ya taa- Tibaijuka | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Hatuna shida ya mafuta ya taa- Tibaijuka

 
Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaujuka amefunguka na kusema kuwa watu wa jimbo lake la Muleba hawana matatizo ya mafuta ya taa bali matatizo makubwa walionayo wao ni magari yao kuharibika kutokana na mafuta aina ya diesel kuchakachuliwa.

Tibaijuka alisema hayo bungeni baada ya kupewa taarifa na Mbunge wa Mbozi (CHADEMA), Pascal Haonga ambaye alikuwa anamwambia Tibaijuka kuwa hata wananchi wake Muleba hawataweza kununua mafuta ya taa kutokana na bei hiyo mpya kwamba itakuwa kubwa sana na kumtaka kurekebisha kauli yake, jambo ambalo Tibaijuka alilikataa na kusema jimboni kwake yeye anapigania magari ya watu yasiharibike.

"Taarifa nimeikataa kwa sababu kule kwangu sisi shida yetu ni magari yasiharibike, engine zisiharibike, kwa hiyo ngoja niwaambie mimi ndiyo nawakilisha watu wangu wa Muleba, matatizo yetu ni disel hata viwanda kama Kagera Sugar karibu kisimame kwa sababu disel inakuwa imechakachuliwa, hivyo uchakachuaji ni mkubwa. Kwa hiyo mafuta ya petroleum ilivyokaa kwenye bajeti ni sawa kabisa" alisema Tibaijuka