F Hii ndio Sababu ya Wabunge wa Upinzani Kumsusia Spika Ndugai Futari | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Hii ndio Sababu ya Wabunge wa Upinzani Kumsusia Spika Ndugai Futari



WABUNGE wa kambi ya upinzani bungeni, jana waliamua kumsusia futari, Spika wa Bunge, Job Ndugai,

Taarifa kutoka kiongozi mmoja mwandamizi kutoka ndani ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) zinasema, uamuzi wa wabunge hao kususia futari umetokana na madai kuwa Spika amekuwa akiendesha Bunge kwa upendeleo.

Hoja ya kususia futari iliwasilisha kwenye kikao kilichofanyika jana kabla ya Bunge kukutana kupitisha bajeti.

“Tulikutana jana na tukakubaliana kwa kauli moja kususia futari hiyo. Hatuwezi kushirikiana na watu wanaotubagua waziwazi,” ameeleza mbunge mmoja wa Ukawa aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina.

Habari zinasema, mbali na mkakati huo, Ukawa umejipanga kukabiliana na serikali hasa kutokana na kauli kuwa “wabunge waliopinga bajeti wanyimwe fedha za maendeleo.”