F Ajali ya daladala na treni yauwa watu wawili | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Ajali ya daladala na treni yauwa watu wawili

Dar es Salaam. Watu wawili wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika  ajali iliyotokea leo asubuhi ikihusisha gari ya abiria aina ya coaster kukigonga kichwa cha treni maeneo ya Yombo Devis Kona.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto amesema  watu wawili wamefariki dunia akiwamo mwanamke mmoja na mwanaume mmoja ambaye ni kondakta wa daladala hiyo.

Muroto amesema mbali na watu wawili kufariki pia kuna majeruhi 36 wanne kati yao wakiwa mahututi.

Amesema majeruhi mahututi ni wanawake watatu na mwanaume mmoja.

“Majeruhi wite wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Temeke na miongoni mwa majeruhi hao wanne wapo katika hali mbaya”amesema Kamanda Muroto.